Bajeti za Rachel Ruto, Dorcas Rigathi na Tessie Mudavadi zaondolewa

Martin Mwanje
1 Min Read

Bajeti zilizokuwa zikitengewa Ofisi za Mke wa Rais Rachel Ruto, Mke wa Naibu Rais Dorcas Rigathi na Mke wa Kinara wa Mawaziri Tessie Mudavadi zimeondolewa. 

Hayo yametangazwa na Rais William Ruto katika hotuba kwa taifa kutoka Ikulu ya Nairobi leo Ijumaa.

Katika maandamano yao wiki mbili zilizopita, vjana wa Gen Z wameshinikiza kuondolewa kwa ofisi hizo wakisema mamilioni ya zinazotengewa zinaweza zikatumiwa kufadhili miradi mbalimbali ya kuwanufaidha Wakenya.

Baadhi ya wanasheria walitilia shaka fedha zinazotengewa ofisi hizo ikizingatiwa kwamba si za kikatiba.

Ofisi hizo zimesemekana kutengewa angalau shilingi milioni 500 kwenye bajeti ili kuendeleza shughuli zake za kila siku.

 

Website |  + posts
Share This Article