Bafana wafurahia kitoweo cha nyangumi na kufuzu kwa nusu fainali AFCON

Dismas Otuke
1 Min Read

Bafana Bafana ya Afrika Kusini ilihitaji ukakamavu wa kipa Ronwen Williams aliyepangua penalti nne, ili kufuzu kwa nusu fainali ya AFCON dhidi ya Cape Verde.

Timu zote zilitoka sare tasa katika robo fainali hiyo ya mwisho Jumamosi usiku baada ya dakika 120 na kulazimu penalti zipigwe kutenganisha miamba hao.

Ilikuwa mara ya kwanza kwa Bafana Bafana kufuzu semi fainali baada ya subira ya miaka 28 huku wakiwinda taji ya pili tangu mwaka 1996.

Afrika Kusini watapambana na Super Eagles ya Nigeria katika nusu fainali Jumatano ijayo.

Share This Article