Burton Mwemba maarufu kama Mwijaku na Clayton Revocatus Chipondo maarufu kama Baba Levo ambao ni watangazaji wa redio nchini Tanzania na ni maarufu ndani na nje ya nchi hiyo kupitia mitandao ni baadhi ya watu walioteuliwa kupigia debe timu za Tanzania kwenye mashindano ya kimataifa.
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo nchini Tanzania Damas Ndumbaro alitangaza uteuzi wa kamati ya wanachama 15 kwa sababu hiyo.
Jukumu kuu la kamati hiyo ni kuhamasisha mashabiki na wanaopenda michezo ndani na nje ya Tanzania kujitokeza kushangilia na kuunga mkono timu za taifa hilo.
Wamejukumiwa pia kuandaa mchango mkubwa wa timu za taifa hafla ambayo inatarajiwa kuandaliwa Januari 10, 2024 katika jiji la Dar es Salaam.
Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa atamwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan kwenye hafla hiyo.
Wajumbe wa Kamati hiyo ni Theobald Sabi ambaye ni mwenyekiti, Patric Kahemela ambaye ni naibu mwenyekiti, Neema Msitha ambaye atakuwa katibu.
Wengine ni Beatrice Singano, Michael Nchimbi, Jemedari Said, Nick Reynolds, Hamis Ali, Christina Mosha, Mhandisi Hersi Said, Salum Abdallah, Paulo Makanza, Mohamed Soloka, Hassan Mohamed Raza, Lucas Mhavile, Oscar Oscar, Prisca Kishamba, Burton Mwemba na Clayton Revocatus Chipondo.