Azimio kutoa mwelekeo Ijumaa

Dismas Otuke
1 Min Read

Muungano wa upinzani wa Azimio la Umoja unatarajiwa kutoa mwelekeo kwa wafuasi wake leo Ijumaa.

Viongozi wa Azimio wataandaa misa ya wafu mtaani Karen kuwakumbuka waliopoteza maisha kwenye maandamano ya siku tatu wiki iliyopita, ambapo baadaye watatoa ratiba na mwelekeo wa harakati zao za kuishurutisha serikali kupunguza gharama ya maisha na utekelezwaji wa sheria ya fedha ya mwaka 2023.

Kiongozi wa upinzani Raila Odinga na viongozi wengine wa upinzani walijitokeza kwa mara ya kwanza mapema wiki hii, tangu maandamano ya siku tatu katika ibada ya kuwakumbuka wafuasi wao wanaodai waliuawa na polisi.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *