Azeeza Hashim ajiunga na Kaka Empire

Marion Bosire
1 Min Read

Mtangazaji Azeeza Hashim ambaye pia hujihusisha na masuala ya kuongoza hafla almaarufu MC amejiunga na kampuni ya mwanamuziki King Kaka iitwayo Kaka Empire Music Label and Recording Company.

Mmiliki na wafanyakazi wa kampuni hiyo walimwandalia Azeeza sherehe ya kumkaribisha usiku wa Jumanne Juni 11, 2024.

Wenyeji walikuwa wamevaa mavazi ya rangi nyeusi huko Azeeza akiwa amevaa rinda la rangi nyeupe. Alipokelewa kwa shada la maua kutoka kwa King Kaka huku wenzake wakimshangilia.

Haijabainika ni jukumu gani atakuwa akitekeleza kwenye kampuni hiyo lakini King Kaka katika tangazo lake kwenye mitandao ya kijamii alimtaja kuwa mtu aliye na talanta katika utangazaji na katika uongozaji wa hafla.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *