Mwigizaji na mchekeshaji wa Nigeria Ayodeji Richard Makun maarufu kama AY alikosa kuhudhuria mazishi ya mamake aliyekuwa mke wake Mabel hali iliyosababisha akashifiwe mitandaoni.
Haijulikani wakati mama Rose Temietan Eyesan Nwanegbu aliaga dunia lakini piacha na video za mazishi yake zimechapishwa mitandaoni.
Watu mbali mbali maarufu nchini Nigeria wameonekana kwenye picha hizo isipokuwa aliyekuwa mume wa Mabel AY Comedian.
Waliohudhuria mazishi hayo katika eneo la Ikoyi jijini Lagos nchini Nigeria ni pamoja na mwanamuziki 2Baba na mkewe Anne Idibia, Waje, mwigizaji Uche Jombo na wengine.
2Baba aliimba wimbo wake maarufu wa ‘Africa Queen’ katika mojawapo ya hafla za mazishi hayo yaliyojaa huzuni.
Watumizi wa mitandao nchini Nigeria wamemkashifu sana AY kwa kutokuwa karibu na aliyekuwa mke wake alipokuwa akiomboleza mamake.
Wametaja kazi ambayo amekuwa akiangazia ya filamu ya ‘The Waiter’ ambayo amehusisha May Yul Edochie mke wa Yul Edochie kuwa isiyofaa.
AY na Mabel walitangaza kuvunjika kwa ndoa yao ya miaka 15 mwezi Aprili mwaka huu wa 2024, baada ya kusherehekea miaka 15 ya ndoa hiyo Novemba 2023.
Wanandoa hao wa zamani wana watoto wawili.
Katika hatua inayokisiwa kuwa ya kujibu wakosoaji wake mitandaoni, AY alichapisha picha akiwa na kakake wakiwa wamevaa mavazi ya rangi nyeusi na kuandika, “It is well …”.
Inaonekana kwamba alihudhuria mazishi hayo hata ingawa hakuonekana kwenye video na picha zilizochapishwa.
Mabel pia anaendelea kutumia jina Makun kwenye akaunti yake ya Instagram ambapo kwenye wasifu anajiita ‘Dr. Mrs. Makun’.