Awamu ya pili ya mradi wa nyumba za gharama nafuu kuanzishwa Nyandarua

Marion Bosire and Lydia Mwangi
1 Min Read
Muchiri Gakuru

Serikali kuu inanuia kuanzisha awamu ya pili ya ujenzi wa nyumba za bei nafuu kwa kima cha shilingi binioni 1.2 mjini Ol kalou katika kaunti ya Nyandarua.

Akizungumza mjini Ol,kalou baada ya mkutano wa kusikiliza na kutoa maoni kuhusu mradi huo, msimamizi wa mradi huu katika eneo la kati mwa nchi Muchiri Gakuru amesema kwamba serikali imejitolea kwa dhati kuhakikisha mradi huo wa ujenzi wa nyumba za gharama nafuu umeimarisha na kuinua hali na hadhi ya wananchi hasa katika miji mikuu ya kaunti na hata vijijini.

Wakati huo huo naibu kamishina wa Kaunti ya Nyandarua ya kati, Michael Ololutuaa amesema kwamba serikali itashirikiana na washika dau mbali mbali kuhakikisha mradi huo unanufaisha watu wengi katika kaunti.

Mikakati maalum pia itawekwa kuhakikisha wananchi wamepata nafasi za kazi wakati mradi huo utakapoanza.

Hata hivyo,Gakuru ameongezea kusema kwamba katika awamu hii ya pili serikali itajumuisha nyumba za kukodi,vyumba vya mikutano, zahanati pamoja na shule za umma.

Website |  + posts
Share This Article