Atwoli achaguliwa tena Katibu Mkuu wa COTU bila pingamizi

Dismas Otuke
1 Min Read

Katibu Mkuu wa muungano wa wafanyakazi nchini COTU Francis Atwoli alichaguliwa bila kupingwa kwenye kikao cha 15, cha mkutano wa kila baada ya miaka mitano ulioandaliwa Jumamosi katika chumba cha Tom Mboya kaunti ya Kisumu.

Ni mara ya sita kwa Atwoli kuchaguliwa kwenye kiti hicho.

Atwoli alichaguliwa kwenye kiti hicho kwa mara ya kwanza mwaka 2001, akirithi mamlaka kutoka kwa Joseph Mugalla.

Maafisa wengine waliochaguliwa bila kupingwa katika nyadhfa zao ni pamoja na Rajabu Mwondi Kasisi, Joel Chebii, Francis Murage, Benson Okwaro, Ernest Nadome, Carolyne Rutto, Rebecca Nyathogora, Wasington Adongo, Francis Wangara, Joseph Nyabiya, na Nelson Mwaniki.

Share This Article