Atletico waizima Real derby ya Madrid

Dismas Otuke
1 Min Read

Atletico Madrid wakicheza nyumbani walivunja rekodi ya Real Madrid ya kutopotezs mechi msimu huu,katika derby ya Jumapili usiku walipoilaza mabao 3 kwa moja mchuano wa ligi kuu.

Álvaro Morata alitikisa nyavu za watani wao mara mbili katika derby hiyo ya 233 huku Antoine Griezman akiongeza jingine moja.

Eduardo Camavinga alipiga goli la kufutia machozi kwa vijana wa Carlo Ancelotti.

Ulikuwa ushindi wa kwanza kwa Atletico wanaonolewa na Diego Simeoni ndani ya mechi 9 zilizopita.

Website |  + posts
Share This Article