Atalanta Bargamo ndio mabingwa wa kombe la Europa League kwa mara ya kwanza baada ya kuwatitiga Bayer Leverkusen ya Ujerumani, mabao matatu kwa nunge katika fainali kali iliyosakatwa Jumatano usiku uwanjani Dublin katika Jamhuri ya Ieland.
Mshmabulizi wa Nigeria Ademola Lookman alipiga magoli mawili ya mwanzoni mwa kipindi cha kwanza, na kudumisha uongozi huo hadi mapumzikoni.
Licha ya Lverkusen kujaribu kurejea mchezoni kunako kipindi cha pili mabeki wa Atalanta walikaa ngumu, huku Lookman akizidisha masaibu kwa kubusu nyavu kwa mara ya tatu.
Atalanta pia walivunja rekodi ya mabingwa hao wa Ujerumani ya kucheza mechi 51 bila kupoteza.