Arsenal walisherehekea kurejea katika kipute cha Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya kwa mara ya kwanza, baada ya subira ya miaka 6 kwa ushindi mkubwa wa mabao 4 kwa bila nyumbani Emirates dhidi ya mabingwa wa Uholanzi PSV Eindhoven Jumatano usiku katika mchuano wa kundi B.
Bukayo Saka, Leandro Trossard, Gabriel Jesus na Martin Odegaard walipachika goli moja kila mmoja.
Katika pambano jingine la kundi hilo, mabingwa wa Europa League, Sevilla walilazimshwa kutoka sare ya 1-1 dhidi ya Lens ya Ufaransa.
Katika kundi B, Manchester United walicharazwa mabao 4-3 na Bayern Munich ugani Allianz.
Leroy Sane, Serge Gnabry,H arry Kane na Mathy’s Tel wakifunga mabao ya Baverians huku wageni wakufungiwa na Casemiro aliyenusu nyavu mara mbili kuongezea kwa bao la ufunguzi lake Rasmus Hojland.
Nchini Uhispania, Real Madrid walihitaji bao lake Jude Bellingham kunako dakika ya mwisho kuwabwaga visirani Union Berlin.