Gabriel Jesus alicheka na nyavu mara tatu kunako kipindi cha pili huku washika bunduki wa Arsenal wakitoma nyuma na kulazimisha ushindi wa mabao 3-2 dhid ya Crystal Palace katika mojawapo ya robo fainali tatu za kombe la Carabao jana Jumatano usiku.
Liverpool pia walitinga nusu fainali kufuatia ushindi wa mabao 2-1 ugenini St. Marys dhidi ya Southampton, wakati Newcastle United ikiwapiku Brentford 3-1.
Manchester United watakuwa ugenini London leo kwa robo fainali ya mwisho dhidi ya Tottenham Hostpur.