Huku wanawake na mashirika ya kijamii wakiandamana leo Jumamosi kulalamikia kuongezeka kwa visa vya mauaji ya wanawake, mwanamke mwenye umri wa miaka 25 kutoka kijiji cha Chemoset, eneo bunge la Belgut kaunti ya Kericho, ndiye mhasiriwa wa hivi punde wa mauaji dhidi ya wanawake.
Mwanamke huyo aliuawa na mumewe mwenye umri wa miaka 27, siku moja tu baada ya kwenda kwa wazazi wake kufuatia mzozo uliozuka wa nyumbani.
Mwanaume huyo anadaiwa kumdunga kisu shingoni. Inasemekana kwamba mwanamke huyo alitofautiana na mumewe baada ya kumwomba ajiunge na chuo.
Mshukiwa huyo alikamatwa na kupelekwa katika kituo cha polisi Sosiot,akisubiri kupelekwa mahakamani.
Mbunge wa kaunti ya Kericho Beatrice Kemei alikashifu kisa hicho,akitoa wito kwa wananume kukomesha kuwaua wanawake.