Antonio Conte ambaye ni meneja wa zamani wa klabu za Uingereza Chelsea na Tottenham Hotspurs, ameteuliwa kuwa kocha mpya wa klabu ya Napoli kwa mkataba wa miaka mitatu.
Meneja huyo wa umri wa miaka 54, hajafanikiwa kusimamia klabu yoyote tangu alipoondoka Spurs mwezi wa Machi 2023.
Licha ya kukuwa na wakati wa kusikitisha huko Uingereza, Conte alishinda Ligi kuu ya Uingereza katika msimu wake wa kwanza na klabu ya Chelsea msimu wa 2016-17 na Kombe la FA katika msimu wake wa pili kabla ya kutimuliwa mwaka wa 2018.
Kando na hayo, meneja huyo wa Kiitaliano amefanikiwa kushinda mataji manne ya ligi ya Serie A, matatu akiwa na klabu ya Juventus na moja akiwa na Inter Milan mnamo 2021.
Mkataba wa Conte na Napoli ni wa thamani ya euro milioni nane kila msimu.