Modeli maarufu Anok Yai amesema hataki tena tuzo ya Modeli bora baada ya kushindwa kwenye tuzo hiyo na Alex Consani aliyezaliwa mwanaume na kujibadilisha kuwa mwanamke.
Alex Consani, wa umri wa miaka 21, ndiye mwanamke wa kwanza aliyejibadili kutoka jinsia ya kiume kuwahi kushinda tuzo hiyo kwenye tuzo za mitindo ya mavazi mwaka huu Disemba 2,.
Consani alipokuwa akitoa hotuba baada ya kutangazwa mshindi, alisema ushindi wake ni hatua kubwa sana katika upande unaofaa.
Anok Yai, wa miaka 26, alimpongeza Consani kupitia ujumbe aliochapisha kwenye mtandao wa X siku moja baadaye akisema hataki tuzo kutoka kwa baraza la mitindo ya mavazi la Uingereza tena.
“Alex, ninakupenda na ninajivunia ufanisi wako. Baraza la mitindo ya mavazi la Uingereza asante lakini siitaki tena.” aliandika binti huyo.
Yai modeli wa Amerika ambaye ndiye wa kwanza wa asili ya Sudan Kusini na wa pili wa asili ya Afrika kuwahi kufungua maonyesho ya Prada alisema pia kwamba amechoka na ushinde lakini anampongeza Consani.
Alisema ameshuhudia juhudi za Alex ndiposa anampongeza.
Anok Yai aliteuliwa kuwania tuzo hiyo pamoja na wengine ambao ni Alva Claire, Amelia Gray, Liu Wen na Mona Tougaard.
Aliteuliwa tena kwa tuzo hiyo hiyo mwaka jana ambapo aliibuka wa pili huku Paloma Elsesser akiibuka mshindi.