Takriban shule 2,000 kukosa kufungua kwa muhula wa pili Jumatatu

Dismas Otuke
1 Min Read

Angaa shule 2,155 huenda zikakosa kufungua kwa muhula wa pili Jumatatu Mei 13 ilivyopangwa.

Waziri wa Elimu Ezekiel Machogu, amesema huenda asilimia tano ya shule nchini zikakosa kufungua Jumatatu ilivyotangazwa na Rais William Ruto wiki iliyoppita, baada ya madarasa kuharibiwa vibaya na maji ya mafuriko.

Nyingi ya shule hizo zinapatikana katika kaunti za Tana River ,Homa Bay na Kisumu.

Shule hizo zitahitaji ukarabati wa majengo, kabla ya kufungualiwa tena kwa masomo.

Shule zote nchini zilipangiwa kufunguliwa April 29 kabla ya siku ya ufunguzi kuahirishwa kwa juma moja kutoka na mafuriko yaliyoshuhudiwa katika maeneo mengi nchini

Share This Article