Amri ya kutotoka nje yatangazwa katika jimbo la Kano, Nigeria

Tom Mathinji
1 Min Read
Amri ya kutotoka nje yatangazwa katika jimbo la Kano nchini Nigeria. Picha/Hisani

Amri ya kutotoka nje imetangazwa katika jimbo la pili kwa ukubwa nchini Nigeria, Kano, kufuatia maandamano ya kupinga gharama ya juu ya maisha, ambayao yanasemekana kuingiliwa na wahalifu.

Afisi ya Gavana wa Kano, ilisema wahuni hao wamehusika katika uharibifu na uporaji wa mali.

Kano ilishuhudia umati mkubwa zaidi katika siku ya kwanza ya maandamano ya kitaifa ambayo yalilazimu biashara nyingi kufungwa.

Waandamanaji katika majiji yote makubwa waliingia barabarani, wakiimba kauli mbiu kama vile: “Tuna njaa.”

Polisi walitumia risasi na vitoa machozi kuwatawanya maelfu ya wandamanaji hao kwenye mji wa Kano.

Watu wanne walijeruhiwa na kupelekwa hospitalini.Waporaji walivunja bohari moja karibu na makao ya gavana wa jimbo hilo na kupora mafuta ya kupika pamoja na magodoro.

Sheria hizo za kutotoka nje zimethibiti hali hiyo huku wakazi wote wakitakiwa kusalia manyumbani kwao.

Mikutano ya hadhara imekuwa ikifanyika katika miji mikubwa nchini kote na vijana wa Nigeria wakiitaka serikali kushughulikia matatizo ya kiuchumi na kurejesha ruzuku ya mafuta ambayo ilitupiliwa mbali mwaka jana.

TAGGED:
Share This Article