Ruben Amorim anatarajiwa kuzinduliwa kuwa meneja mpya wa klabu ya Manchester United kabla ya mwishoni mwa juma hili kumrithi Erik Ten Hag, aliyeenguliwa mapema wiki hii.
Kulingana na Afisa Mkuu Mtendaji wa Man U Dave Brailsford, Amorim aliafikiana kuhusu mkataba na masharti ya utendakazi jana.
Kocha huyo mpya anatarajiwa kuwa uwanjani wakati Man U itawaalika Chelsea Jumapili hii katika mechi ya Ligi Kuu Uingereza.
Hadi uteuzi wake, Amorim amekuwa meneja wa klabu ya Ureno ya Sporting Lisbon.