Kocha wa klabu ya AFC Leopards Fred Ambani na mshambulizi wa Posta Rangers Jackson Macharia, wametawazwa kocha na mchezaji bora wa mwezi Machi, katika Ligi ya Sportpesa humu nchini.
Ambani aliiongoza Ingwe kuinyuka Shabana FC mabao 5-1,lakini wakabinikizwa magoli 4-1, dhidi ya Mathare United.
Mchezaji huyo wa zamani wa Harambee Stars alituzwa shilingi 75,000, kwa ushindi huo ,ikiwa mara ya pili kunyakua tuzo hiyo ligini msimu huu.
Macharia kwa upande wake alipachika magoli 4 katika mechi nne za mwezi uliopita na amepewa zawazi ya shilingi 50,000.