Nelson Mahanga Mwita ambaye awali alihudumu kama Naibu Gavana katika kaunti ya Migori amefariki.
Familia yake imethibitisha kifo chake na kufafanua kwamba alikata roho jana Jumamosi akipokea matibabu katika hospitali ya MP Shah Hospital, Nairobi.
Mahanga alikuwa Naibu wa Gavana Okoth Obado kati ya mwaka 2013 na mwaka 2022.
Gavana wa sasa wa Migori Ochillo Ayacko alitangaza kifo cha Mahanga kupitia mtandao huku akitoa rambirambi kwa ndugu jamaa na marafiki.
Mwili wa marehemu unahifadhiwa katika makafani ya Lee jijini Nairobi.