Aliyekuwa Mkuu wa vikosi vya KDF Robert Kibochi ateuliwa serikali

Tom Mathinji
1 Min Read
Aliyekuwa Mkuu wa vikosi vya Ulinzi KDF, Rovert Kibochi.

Rais William Ruto amemteua aliyekuwa Mkuu wa vikosi vya ulinzi nchini KDF, Jenerali mstaafu Robert Kibochi, kuwa mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi ya hospitali ya rufaa ya Mwai Kibaki.

Uteuzi wa Kibochi ulitangazwa kupitia gazeti rasmi la serikali la Novemba 22,2024.

Kibochi atahudumu katika wadhifa huo kwa muda wa miaka mitatu, huku uteuzi wake ukitekelezwa mara moja.

Wakati huo huo, kiongozi wa taifa pia alimteua aliyekuwa mbunge wa Rarieda Nicholas Gumbo, kuwa mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi ya sukari nchini, huku aliyekuwa mbunge wa Kesses Swarup Mishra, akiteuliwa mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi ya taasisi ya Biovax hapa nchini.

Wawili hao pia watahudumu kwa kipindi cha miaka mitatu.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *