Aliyekuwa kiongozi wa Mungiki Maina Njenga alikamatwa na maafisa wa polisi Jumatano usiku.
Kulingana na wakili wake Ndegwa Njiru, Njenga alikamatwa pamoja na kakake Njoroge Njenga na msaidizi wao Ole Lekishe. Wote hao walikamatwa katika sehemu ya Kiserian na kisha kupelekwa katika sehemu isiyojulikana.
“Mteja wangu Maina Njenga alikamatwa na kupelekwa mahali kusikojulikana,” aliandika Njiru katika mtandao wake wa Twitter.
Kulingana na familia yake, maafisa wa usalama walifika nyumbani kwake Jumatano mwendo waa mbili unusu usiku na kuwakamata watatu hao huku baadhi ya maafisa wa usalama wakibaki na kupekua nyumba yake.
Aidha haijabainika kiini cha kukamatwa kwa Maina Njenga.
Kukamatwa kwa Njenga kunajiri siku ya kwanza ya maandamano yaliyoitishwa na upinzani.