Alien Skin alaumiwa kwa kuvamia afisi za chama cha NUP

Alien Skin na wenzake wanadaiwa kuvamia afisi hizo za NUP katika eneo la Kavule saa tisa alfajiri jana Jumamosi na kutishia mlinzi.

Marion Bosire
2 Min Read
Alien Skin, Mwanamuziki Uganda

Chama cha mwanamuziki na mwanasiasa wa Uganda Bobi Wine cha National Unity Platform – NUP kinalaumu mwanamuziki Patrick Mulwana anayejulikana sana kama Alien Skinkwa kuvamia makao makuu ya chama hicho.

Alien Skin na wenzake wanadaiwa kuvamia afisi hizo za NUP katika eneo la Kavule saa tisa alfajiri jana Jumamosi na kutishia mlinzi.

Skin na kundi lake wanadaiwa kuvuruga afisi hizo na kuchora michoro isiyo mizuri kwenye kuta, kulingana na maelezo yaliyotolewa na Bobi Wine.

“Inasikitisha kuona kwamba hawa ndugu hawajajifunza lolote kutokana na hali za waliotumiwa awali na utawala wa nchi hii.” alisema Wine kwenye taarifa yake katika kitandazi cha X.

Alitaja wanamuziki kama Sipapa, Sobi, Zebra na Kitatta kama waliotumiwa na utawala awali.

“Ni huzuni kwamba kila mara tunapokaribia uchaguzi, kuna kundi ambalo liko tayari kuhusika katika uhalifu dhidi ya watu.” aliendelea kusema Wine.

Alimalizia kwa kusema kwamba wanatumai kwamba Skin na kundi lake watajirudi kabla muda haujasonga sana.

Mwezi uliopita Alien Skin aliachiliwa kutoka kwa jela ya Luzira ambako alikaa kwa wiki kadhaa kwa madai ya kuiba simu aina ya Iphone 15 Pro-max na kuvamia wahudumu katika hospitali ya Nsambya.

Siku chache baadaye alihusika kwenye uzinduzi wa chama cha Democratic Alliance – DA kinachoongozwa na aliyekuwa kiongozi wa upinzani Mathias Mpuuga aliyefurushwa kutoka chama cha NUP.

Mpuuga alifukuzwa NUP kwa sababu ya utata kuhusu jinsi alitengewa shilingi milioni 500 pesa za Uganda kama tuzo ya utendakazi.

Alien Skin alitia saini mkataba na chama hicho kipya cha DA katika harakati za chama hicho za kuvutia wafuasi zaidi na kumshinda Rais Museveni katika uchaguzi ujao.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *