Akothee aashiria kwamba atafunga ndoa kwa mara nyingine

Kulingana naye hiyo ndoa ya tatu huenda ikawa ya mwisho lakini isipofanikiwa basi kutakuwa na nyingine.

Marion Bosire
1 Min Read

Mwanamuziki Esther Akoth Kokeyo maarufu kama Akothee ameashiria kwamba huenda akaingia kwenye ndoa kwa mara nyingine.

Alichapisha picha zake za harusi mbili za awali na kuandika, “KUOLEWA KWA AKOTHEE NI CONSTANT” huku akisema harusi ya tatu na ambayo huenda ikawa yake ya mwisho itakuwa bora zaidi.

Kulingana na Akothee ndoa hiyo itakuwa na mpenzi wake Nelly Oaks huku akirejelea waume zake wa awali kuwa wahalifu wa mapenzi.

Lakini tena alijichanganya alipoongeza kusema, “Hii sasa ni ya kweli. Na hii ya tatu isipofanikiwa tutakuwa na nyingine ya mwisho, wewe kazi yako iwe ni kushona kitenge na bundles”.

Akothee aliwahi kufanya harusi na Jared Okello na Denis Schweizer, ndoa ambazo hazikufanikiwa.

Ameendelea kumsifia Nelly Oaks akisema wamekuwa pamoja kwa miaka kumi na watazidi kuwa pamoja.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *