AK yabadilisha kikosi cha mbio za Relay kufuzu kwa mashindano ya dunia

Dismas Otuke
1 Min Read

Chama cha riadha nchini, AK kimelazimika kufanya mabadiliko kwenye timu ya mita 400 ya wanariadha wanne kupokezana kijiti ya Kenya iliyokuwa isafiri kwenda Ujerumani kuwania kufuzu mashindano ya riadha duniani siku ya Jumamosi.

AK wamelazimika kuwajumuisha kikosini Boniface Mweressa na Naomi Korir kutwaa nafasi za Zablon Ekwam na Millicent Ndoro baada ya wawili hao kukosa vyeti vya usafiri kwa wakati.

Pia kocha wa mbio za masafa mafupi Duncan Ayiemba aliyekuwa aandamane na timu alibadilishwa huku nafasi yake ikitwaliwa na Perpetua Mbutu.

Timu ya Kenya ya mbio za masafa mafupi iliondoka nchini na inawajumisha mabingwa wa Jumuiya ya Madola Wyclif Kinyamal, Mary Moraa, Boniface Mweresa na Naomi Korir.

Kenya inaorodheshwa ya 16 katika mbio hizo za kupokezana kijiti na endapo watadumisha nafasi hiyo kwenye msimamo wa dunia kufikia Julai 31, watafuzu kwa mashindano ya riadha ulimwenguni.

Makala ya 19 ya mashindano ya riadha ulimwenguni yataandaliwa mjini Budapest, Hungary kati ya Agosti 19 na 27 mwaka huu.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *