AK kuchagua wanariadha 30 kwa michezo ya Afrika

Dismas Otuke
1 Min Read

Chama cha Riadha nchini AK kitachagmmmm ua wanariadha 30 watakaowakilisha Kenya kwa makala ya 13 ya michezo ya Afrika itakayoandaliwa mjini Accra Ghana kunzia Machi 8 hadi 23.

Kulingana na naibu Rais wa chama cha Riadha Paul Mutwii, Baraza Kuu la Michezo nchini limetenga nafasi 30 kwa wanariadha watakaoiwakilisha Kenya.

Majaribio ya kitaifa yameratibiwa kuandaliwa kati Machi 5 na 6 uwanjani,  ambapo mwanariadha mmoja atachaguliwa kutoka kila fani .

Mutwii alikariri kuwa ni wanariadha pekee watakaoalikwa na kutimiza vigezo vya Shirika la kupambana na ulaji muku wakiwa wanaume 16 na wanawake 14,watajumuishwa kwa kikosi cha Ghana.

Huku hayo yakijiri maandalizi yamekamilika kwa  majaribio ya kitaifa ya mbio za nyika  katika uwanja wa chuo cha mafunzo ya askarijela eneo la  Ruiru siku ya Jumamosi tarehe 2 Machi.

Wanariadha sita wa kwanza katika kila fani watajumuishwa kwa timu ya Kenya itakayoshiriki mashindano ya dunia ya mbio za nyika mjini Belgrade,Serbia tarehe 30 Machi.

AK itaandaa mafunzo kwa washiriki wote Ijumaa Machi mosi uwanjani Ruiru.

Watakaoteuliwa wataingia kwenye kambi ya mazoezi kujiandaa kwa mashindano hayo ya Dunia.

Kenya itakuwa ikitetea taji ya jumla nchini Serbia ,baada ya kutawazwa mabingwa mjini Bathurst, Australia, mwaka 2023 .

Website |  + posts
Share This Article