Ahly watoshana nguvu na Esperance

Dismas Otuke
1 Min Read

Washindi mara 10 wa kombe la Ligi ya Mabingwa Afrika,Al Ahly ya Misri walilazimisha sare tasa dhidi ya Esperance ya Tunisia katika duru ya kwanza ya fainali.

Timu zote zilibuni nafasi haba za kufunga mabao katika pambano hilo la Jumamosi usiku mjini Tunisia.

Ahly wanaowania kombe hilo kwa mara 11 watawaalika mabingwa mara nne Esperance, katika mchuano wa marudio Jumamosi ijayo jijini Cairo.

Mshindi atatuzwa dola milioni 1.5 za Marekani na kombe.

Share This Article