Afya ya Waziri Mkuu wa Slovakia Robert Fico haiko hatarini

Dismas Otuke
1 Min Read

Waziri Mkuu wa Slovakia Robert Fico hayuko hatarini kiafya, baada ya kupigwa risasi mara kadhaa Jumatano jioni.

Awali Waziri wa Ulinzi alitoa ripoti kuashiria kuwa hali ya Waziri Mkuu huyo ilikuwa mbaya

Fico alishambuliwa katika mji mdogo wa Handlova na kushambuliwa kwa risasi, katika kile kinachokisiwa kuwa shambulizi linalohusiana na siasa.

Mshukiwa mmoja alikamatwa katika eneo la mkasa akidaiwa kuwa mwanaume wa umri wa miaka 71, ambaye ni mwandishi wa siasa na mwanaharakati.

Shambulizi hilo lilijiri siku moja baada ya bunge kuanza kujadili pendekezo la kufutilia mbali shirika la utangazaji nchini humo RTVS.

Share This Article