Afueni!watakaoshindwa uchaguzi mkuu mwaka ujao kuteuliwa bungeni

Dismas Otuke
1 Min Read
Vikao vya bunge la taifa.

Ni afueni kwa waaniaji wa uchaguzi mkuu katika viti vya Urais na Naibu wake  watakaoshindwa kwani sasa wanaweza kuteuliwa na chama kuwa Wabunge.

Hii ni kufuatia bunge la kitaifa kufanyia marekebisho sheria za tume ya uchaguzi (IEBC)  ya mwaka 2024 ibara ya 9, ambapo sasa wataingia bungeni kupitia uteuzi wa vyama vyao.

Awali sheria ya uchaguzi iliwafungia nje wapeperushaji bendera ya Urais na manaibu wao kutoka vyama vya kisiasa kuteuliwa bungeni.

Hatua hiyo ilifuatia agizo la mahakama lililosema kuwa kuwafungia nje waaniaji hao katika uteuzi wa bunge ni kinyume cha katiba na ukiukaji wa sheria.

Share This Article