Afrika yatakiwa kuunga mkono juhudi zake za udumishaji amani

Tom Mathinji
1 Min Read

Rais mstaafu Uhuru Kenyatta, amesisitiza haja ya mataifa ya Afrika kufadhili na kuunga mkono mikakati ya nchi hizo ya kutatuta migogoro na kudumisha amani.

Uhuru alisema ni muhimi sana kwa Afrika kuongoza mikakati yake ya kudumisha amani, ili kuhakikisha upatikanaji wa suluhu za kudumu.

“Iwapo tunataka suluhu za kudumu ambazo zimetokana na juhudi za Afrika, hatuwezi afikia hayo ikiwa hatutaunga mkono michakato hiyo kupitia rasilimali ambazo tunazalisha,” alisema Uhuru.

Uhuru aliyasema hayo jana Ijumaa wakati wa mkutano wa 15 kuhusu mchakato udumishaji amani, usalama na udhabiti barani Afrika, ulioandaliwa Abidjan, nchini Côte d’Ivoire.

Mkutano huo uliwaleta pamoja viongozi wa ngazi za juu wa tume ya Muungano wa Afrika, wawakilishi maalum, viongozi wa kiucumi wa maeneo pamoja na wajumbe wa kimataifa, kujadili usuluhishaji wa migogoro na mikakati ya kuleta amabi barani Afrika.

Wakati huo huo, Kenyatta alimpongeza mweyekiti wa tume ya Umoja wa Afrika Moussa Faki kwa kubuni hazina ya AU, inayolenga kusaidia operesheni za kuleta amani na kusuluhisha majanga katika bara hilo.

Aidha Kenyatta alielezea umuhimu wa ushirikiano wa kanda, akidokeza kuwa Afrika haiwezi afikia utangamano kamili, ikiwa haitatatua changamoto za kikabila, kidini, migogoro ya rasilimali na mzozo unaotokana na mabadiliko ya tabia nchi.

Share This Article