Afrika Kusini,Morocco na Algeria zawania makao makuu ya CAF

Dismas Otuke
0 Min Read

Mataifa matatu ya Afrika Kusini,Morocco na Algeria yametuma maombi ya kuwania kuwa makao makuu ya shirikisho la soka barani Afrika CAF kurithi Misri.

Misri imekuwa makao makuu ya CAF tangu mwaka 1957 baada ya kutwaa kutoka kwa Sudan.

CAF imeanzisha mfumo mpya wa kudurisha makao makuu yake mara kwa mara kutoka kwa nchi moja hadi nyingine kama njia ya kuashiria uwazi na uwajibikaji.

Share This Article