Afrika Kusini inalenga kuwa taifa la kwanza Afrika kuandaa michezo ya Olimpiki ya mwaka 2036 baada ya kutuma maombi.
Waziri wa Michezo sanaa,na utamaduni Gayton McKenzie alitangaza haya mapema wiki hii mjini Luasanne ,Uswizi akiandamana na maafisa wa kamati ya Olimpiki nchini Afrika Kusini (SASCOC).
Maafisa wa IOC wanatarajiwa kuzuru Afrika Kusini kufanya ukaguzi wa miundo msingi kabla ya uamuzi kutolewa.
Afrika Kusini ilikuwa nchi ya kwanza Afrika kuandaa fainali za Kombe La Dunia mwaka 2010.