Afrika kupokea chanjo dhidi ya ugonjwa wa Mpox

Tom Mathinji
1 Min Read

Kituo cha Afrika cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa (Africa CDC), kimesema kinalenga kuhakikisha chanjo Milioni 10 za chanjo dhidi ya ugonjwa wa Mpox zinapatikana barani Afrika.

Tayari kituo hicho, kimetangaza ugonjwa wa Mpox kuwa dharura ya afya ya umma barani Afrika, kufuatia kuenea haraka kwa ugonjwa huo.

Katika mkutano na wanahabari,  Mkurugenzi Mkuu wa kituo hicho Dkt. Jean Kaseya, alisema chanjo zza ugonjwa huo zitapelekwa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kuanzia wiki ijayo.

Kulingana na kituo hicho cha Africa CDC, Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo huenda ikaanza kuwachanja raia wake dhidi ya Mpox.

Kaseya alitoa wito kwa mataifa ya Afrika kutowaadhibu raia wake kutokana na kuzuka kwa ugonjwa huo, huku kituo hicho kikijizatiti kudhibiti hali.

Share This Article