Huduma ya taifa ya polisi, umesema imemtambua afisa wa trafiki aliyenaswa kwenye kanda ya video akichukua hongo kutoka kwa magari ya uchukuzi wa umma.
Kupitia kwa taarifa kwenye mtandao wake wa X, huduma hiyo ya polisi ilisema imemsimamisha kazi mara moja konstebo Haron Mwangi mwenye nambari ya ajira 63151, ambaye ni afisa ww trafiki katika kituo cha polisi cha Buruburu.
Kulingana na huduma hiyo, taratibu za kumwachisha kazi zinaendelea.
“Afisa wa polisi wa trafiki nambari 6315, wa kituo cha polisi cha Buruburu, amesimamishwa kazi mara moja, huku taratibu za kumwachisha kazi zikiendelea,” ilisema taarifa ya huduma ya taifa ya polisi.
Huduma ya taifa ya polisi imepongeza umma na wanahabari kwa ushirikiano wao katika vita dhidi ya ufisadi.