Afisa wa polisi wa Kenya atoweka nchini Haiti

Tom Mathinji
1 Min Read
Afisa wa polisi wa Kenya, atoweka nchini Haiti.

Afisa wa polisi wa Kenya anayehudumu chini ya kikosi cha kimataifa cha kudumisha usalama nchini Haiti (MSS), ameripotiwa kutoweka.

Habari hizo za kutoweka kwa afisa huyo zimetolewa Jumatano asubuhi, na Huduma ya Taifa ya Polisi (NPS).

Kulingana na NPS, afisa huyo alitoweka Machi 25, 2025 akiwa kazini baada ya shambulizi katika eneo la Pont-Sonde, huku operesheni ya kumtafuta ikiendelea.

“Huduma ya Taifa ya polisi imefahamishwa kwamba afisa wa polisi wa Kenya anayehudumu chini ya kikosi cha kimataifa cha kudumisha usalama nchini Haiti (MMS), ametoweka. MSS, kwa ushirikiano na Huduma ya Taifa ya polici ya Haiti (HNP), zinashirikiana katika operesheni ya kumtafuta afisa huyo,” ilisema taarifa ya NPS.

Wakati huo huo, Huduma ya Taifa ya Polisi, imewapongeza zaidi ya maafisa 600 wa polisi wa Kenya wanaokabiliana na makundi ya wahalifu nchini Haiti.

“Tunawapongeza maafisa wa polisi wanaohudumu nchini Haiti, ambao wako imara kutekeleza majukumu ya kikosi cha kimataifa cha kudumisha usalama nchini Haiti,” iliongeza taarifa hiyo ya NPS.

Haya yanajiri siku chache baada kuuawa kwa afisa wa polisi wa Kenya aliyekuwa akihudumu nchini Haiti, konstebo Samuel Tompoi, aliyezikwa juma lililopita.

Website |  + posts
TAGGED:
Share This Article