Afisa wa polisi wa bunge akamatwa kwa ulaghai

Marion Bosire
1 Min Read

Afisa wa polisi aliye katika Kituo cha Polisi cha Bunge anakabiliwa na mashtaka ya ufisadi kwa kujaribu kuitisha rushwa ya shilingi 40,000 kutoka kwa mshukiwa aliyekuwa na kesi isiyokamilika.

Mlalamikaji alikamatwa na polisi kituoni hapo lakini DPP alipopokea jalada hilo, ili kuridhia upande wa mashtaka badala yake aliamuru aachiwe huru, huku akiagiza shauri hilo kumalizwa nje ya mahakama.

“Hata hivyo, John Mwai Mbili alimwambia mlalamikaji kwamba lazima amlipe “kitu kidogo” ili “kuwezesha kufungwa” kwa suala hilo. Alidai rushwa kutoka kwa mlalamishi akitishia kwamba ikiwa mlalamishi atakosa kulipa, atamshtaki kortini kwa makosa mapya,” EACC ilisema kwenye taarifa yake kupitia X.

“Mlalamishi aliripoti suala hilo kwa EACC ambayo ilifanya uchunguzi na baadaye kumkamata afisa wa polisi” iliongeza.

Afisa huyo alipelekwa katika Kituo cha Polisi cha Integrity Centre ambako alishughulikiwa na baadaye kufikishwa katika Kituo cha Polisi cha Kilimani.

Mwai ameachiliwa kwa dhamana akisubiri kukamilika kwa vipengele vilivyosalia vya upelelezi.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *