Afisa wa polisi ampiga hakimu risasi mahakamani Makadara, Nairobi

Marion Bosire
0 Min Read

Afisa wa polisi anaripotiwa kumpiga risasi na kumuumiza hakimu wa mahakama ya Makadara, Nairobi.

Polisi huyo alikuwa amefika mahakamani kwa ajili ya kusikilizwa kwa kesi ya mkewe anayeripotiwa kuhukumiwa kifungo cha maisha gerezani na mahakama ikakataa kumwachilia kwa dhamana.

Maafisa wa polisi waliokuwa wakishika doria mahakamani wanasemekana kujibu haraka na kumpiga risasi afisa huyo wa polisi.

Afisa huyo pamoja na hakimu walikimbizwa hospitalini.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *