Afisa mmoja mkuu wa halmashauri ya ukusanyaji ushuru nchini, KRA amekanusha madai ya kukutana na mfanyabiashara Ann Njeri.
Njeri anadai kuagiza shehena ya tani laki moja za mafuta ya dizeli kutoka nchini Urusi ya thamani ya shilingi bilioni 17, madai ambayo serikali imeyapuuzilia mbali.
Mfanyabiashara huyo alidai kukutana na afisa mmoja mkuu wa KRA kuhusu shehena hiyo, madai ambayo pia afisa huyo amekanusha.
Kesi ya Njeri kuhusu utata unaozingira umiliki wa shehena hiyo ilianza kusikizwa jana Jumatano katika mahakama moja ya Mombasa.
Waziri wa Nishati Davis Chirchir amesimama kidete kusema kuwa Njeri alighushi stakabadhi za kuagiza mafuta hayo na wala sio mmiliki wa shehena hiyo.