Osman Khalif ambaye ni Msaidizi wa Gavana wa Nairobi Johnson Sakaja, aliyeripotiwa kuwa ametoweka siku 17 zilizopita amepatikana.
Mnamo siku ya Jumatatu, wakili wa familia ya Khalif alimwambia Justice Chacha Mwita kwamba, Khalif alipatikana na alipelekwa hospitalini kwa uchunguzi wa matibabu na sasa anapata nafuu akiwa nyumbani.
Hata hivyo wakili huyo amesema wanahitaji muda zaidi wa kupata mwelekeo, alidokeza kuwa uchunguzi lazima ufanyee kuwatambua waliomshika mateka Khalif na lengo lao lilikuwa ni lipi.
Hii ni baada ya afisi ya Inspekta mkuu wa polisi na idara ya upelelezi wa maswala ya jinai DCI kutaka kesi hiyo iondolewe.
kupatikana kwa Khalif kunajiri wiki mbili baada ya Mahakama kuagiza huduma ya taifa ya polisi kuwatia nguvuni waliomshika mateka Khalif.