Afisa wa Kaunti adaiwa kuuawa na yaya Kilifi

Marion Bosire
1 Min Read

Afisa mkuu wa serikali ya kaunti ya Kilifi ambaye alikuwa anasimamia masuala ya uvuvi na uchumi wa baharini Rahab Karisa ameaga dunia.

Karisa anasemekana kuuawa kwa kudungwa kisu na mhudumu wake wa nyumbani huko Mnarani, kaunti ya Kilifi leo Alhamisi asubuhi.

Alirejea kutoka nchini Italia Jumatano ambako alikuwa amekwenda kwa ziara.

Mfanyakazi huyo wa nyumbani anaripotiwa kutoroka kabla ya kuwasili kwa walinzi wa kibinafsi baada ya kutekeleza kitendo hicho cha kinyama.

Maafisa wa polisi wameanzisha uchunguzi.

Ripoti yake Dickson Wekesa

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *