Afisa bandia wa EACC anaswa kwa kutapeli Wakenya

Dismas Otuke
0 Min Read

Tume ya maadili na kupambana na ufisadi nchini Kenya EACC,imemkamata jamaa ambaye amekuwa akitapeli umma akijidai kuwa Mkurugenzi wa kijasusi wa tume hiyo.

EACC ilifanya uchunguzi kufuatia malalamishi kadhaa ya kutoka kwa umma wakisema kuwa jamaa huyo amewatapeli

Mshukiwa huyo anadaiwa kutapeli umma mamilioni ya pesa alipojidai kufanya uchunguzi dhidi ya ufisadi, akiahidi kuwasaidia kutokamatwa.

Mshukiwa huyo amekamatwa na vyeti na stakabadhi ghushi za EACC .

TAGGED:
Share This Article