Makala ya 20 ya kindumbwendumbwe cha Kombe la mataifa ya Afrika AFCON, kwa chipukizi chini ya umri wa miaka 17, kitaanza rasmi leo usiku nchini Morocco huku mataifa 16 yakiwania taji.
Ni mara ya kwanza kwa kipute hicho kujumuisha mataifa 16 huku timu kumi bora zikifuzu kwa fainali za Kombe la Dunia zitakazoandaliwa Novemba mwaka huu nchini Qatar.
Wenyeji Morocco watafungua dimba kundini A dhidi ya Uganda kaika uchanjaa wa Mohammédia kuanzia saa nne usiku, kabla ya Zambia kumenyana na Tanzania kesho kuanzia saa nane adhuhuri .
Pia mechi za kundi B zitaanza kesho, Burkina Faso, wakikabiliana na Cameroon kuanzia saa kumi na moja jioni katika uwanja wa Casablanca, kisha Misri wakamilishe raundi ya kwanza kundini B dhidi ya Afrika Kusini.
Kundo C linawajumuia mabingwa watetezi Senegal, Gambia, Somalia na Tunisia huku Mali, Angola, Côte d’Ivoire na Jamhuri ya Afrika ya Kati zikisheni kundi D.