Hafla za mwaka huu za mchezaji bora barani Afrika zitaandaliwa Jumatatu Disemba 16 mjini Marrakech Morocco,ikiwa mwaka wa pili mtawalia kwa tuzo hizo kuandaliwa katika mji huo wa kitalii.
Tuzo ya mwanasoka bora wa mwaka kwa wanaume inawindwa na Simon Adingra wa Cote d’Ivoire na Brighton & Hove Albion,Serhou Guirassy wa Guinea na Borussia Dortmund,Achraf Hakimi kutoka Morocco na Paris Saint-Germain,Ademola Lookman wa Nigeria na Atalanta na Ronwen Williams kipa wa Afrika Kusini na klabu ya Mamelodi Sundowns.
Wanaowania tuzo ya wanawake ni :Sandrine Niyonkuru wa Burundi,Tabitha Chawinga naTemwa Chawinga wote kutoka Malawi Sanaâ Mssoudy wa Morocco ,Chiamaka Nnadozie na Rasheedat Ajibade kutoka Nigeria,Jermaine Seoposenwe na Thembi Kgatlana wa Afrika Kusini na Barbra Banda na Racheal Kundananji wote kutoka nchini Zambia.
Tuzo nyinginezo ni Klabu bora,Kipa bora,Kocha bora ,timu bora ya taifa na mchezaji bora miongoni mwa wanaopiga soka barani.