Adani yasaini mkataba wa shilingi bilion 95.6 na KETRACO

Dismas Otuke
1 Min Read

Kampuni ya KETRACO imesaini mkataba wa kima cha shilingi bilioni 95.68 na kampuni ya Adani Energy Solutions kwa kipindi cha miaka 30.

Kulingana na Waziri wa Nishati Opiyo Wandayi, kampuni ya Adani Energy Solutions itasimamia na kuendesha shughuli za KETRACO kwa kipindi cha miaka30 ijayo.

Kulingana na Waziri Wandayi ushirikiano huo utawezesha kuongezeka kwa kiwango cha umeme na kuboresha miundo mbinu ya umeme nchini.

Wandayi ameongeza kuwa serikali haigharamika kwa vyovyote katika mkataba huo.

Share This Article