ADAK yanusurika kutoka kwa meno ya WADA

Dismas Otuke
1 Min Read

Ni afueni kwa ya muda kwa shirika la kupambana na ulaji muku nchini ADAK, baada ya shirika la kukabiliana na shirika la kuzuia matumizi ya dawa za kuongeza nguvu mwilini (WADA) kusitisha utekelezwaji wa vikwazo baada ya Kenya kutajwa kutozingatia sheria za WADA.

Kwenye taarifa ya jana WADA ilitangaza kusitisha vikwazo kutoka na hatua zilizopigwa na Kenya katika kipindi cha miezi minne kilichotajwa kwenye ripoti ya uchunguzi ya mwezi mei mwaka jana.

WADA badala yake imependekeza kesi ya Kenya kuchunguzwa na kamati huru kabla ya ripoti kuwasilishwa kwa kamati kuu.

Hatua hii ina maana kuwa ADAK, itaendelea kupokea ufadhili na manufaa yote kutoka kwa WADA huku pia maombi ya Kenya ya kuandaa mashindano ya Riadha Dunia mwaka 2029 na 2032 yakipata afueni.

Miongoni mwa mapendekezo ya WADA ambayo Rais William Ruto amekubali kutekeleza ni pamoja na kubadilisha mfumo wa shirika la ADAK na kuongoeza pesa zinazotengewa kwa shughuli za kukabiliana na ulaji muku nchini

Website |  + posts
TAGGED:
Share This Article