Gavana wa kaunti ya kwale Fatuma Achani ameshikiniza serikali ya kitaifa kuharakisha mpango wa kutoa mirabaha ya shilingi billioni 1.2 inayotokana na faida za uchimbaji madini na kampuni ya Base Titanium kwa kipindi cha miaka 10 hadi kufikia sasa.
Achani aliyekuwa akizungumza katika halfa ya kufungua shule ya chekechea ya Miguneni huko Kasemeni katika eneo la Kinango, amekosoa hatua ya bunge la kitaifa kuondoa jumla ya shilingi millioni 650 katika bajeti ya mwaka 2024/2025 fedha zilizotarajiwa kukabidhiwa kaunti ya kwale kama ruzuku ya madini.
Gavana huyo ameongeza kuwa licha ya kampuni ya base titanium kuendeleza shughuli za uchimbaji madini kwale kwa Muda wa miaka 10 wakazi wa kwale bado hawajaona faida zake.
Kampuni ya base titanium inatarajiwa kukamilisha shughuli za uchimbaji madini mwishoni mwa mwaka huu.
Serikali ya kitaifa ilitarajiwa kukabidhi serikali ya kaunti ruzuku ya madini kiawamu Achani akitamaushwa na serikali ya kitaifa kutoipatia kaunti ya kwale ruzuku ya madini (royalities).