Beki wa Kenya Police FC Abud Omar ameteuliwa kuwa nahodha Harambee Stars kwa michuano ya Mapinduzi Cup.
Mashindano ya kuwania Kombe la Mapinduzi yanaandaliwa kisiwani Zanzibar kuanzia leo hadi tarehe 13.
Mechi zitachezwa kwa mfumo wa Ligi kufuatia kujiondoa kwa Burundi na Uganda, kumaanisha kuwa ni mataifa manne pekee yaliyosalia ya Zanzibar, Tanzania bara, Burkina Faso na Kenya.
Ni mara ya kwanza kwa Omar kuvalia mkanda wa unahodha baada ya kuichezea Kenya kwa muda mrefu.
Stars itafungua michuano ya Mapinduzi kesho usiku dhidi ya The Stallions ya Burkina Faso, kabla ya kuvaana na Kilimanjaro Stars ya Tanzania Jumanne ijayo na kuhitimisha ratiba na Zanzibar Heroes Ijumaa ijayo.