Kampuni ya Kenya Airways imesema kuwa abiria mmoja aliyekuwa akisafiri kutoka mjini New York, Marekani, kuja Nairobi jana alifariki ndege ikiwa safarini.
Kulingana na taarifa ya KQ, mkasa huo ulitokea katika ndege ya KQ 003, iliyosafiri kutoka uwanja wa John F. Kennedy mjini New York, kuelekea uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi.
Licha ya matabibu wa ndege kujaribu kutoa huduma ya kwanza, abiria huyo alifariki saa tatu na dakika 10 asubuhi kabla ya ndege kutua.
Kulingana na taarifa ya KQ, ndege hiyo ilijaribu kutua katika uwanja wa Entebbe nchini Uganda, lakini abiria huyo aliripotiwa kufariki kabla ya ndege kutua.