Abiria afariki baada ya magari mawili kushambuliwa Moyale

Tom Mathinji
1 Min Read
Watu wawili wafariki baada ya magari mawili kushambuliwa kwenye barabara kuu ya Moyale - Nairobi.

Mtu mmoja amefariki na wengine watatu kujeruhiwa vibaya baada ya basi walimokuwa wakisafiria kushambuliwa na watu wasiojulikana. 

Basi la kampuni ya Salama lilikuwa likisafiri kutoka Moyale kuelekea Nairobi, lilishambuliwa Jumatatu usiku kati ya eneo la Bori na Dadach Lakole, katika kaunti ndogo ya Moyale, kaunti ya Marsabit.

Shambulizi hilo, lilisababisha majeraha mabaya kwa abiria wanne, wote ambao walipelekwa katika hospitali ya Sololo kwa matibabu, ambapo mmoja aliaga dunia akipokea matibabu.

Muda mfupi baada ya basi hilo kushambuliwa, gari aina ya Toyota Land Cruiser, lililokuwa likisafiri katika barabara hiyo hiyo, lilishambuliwa na wavamiszi hao.

Mmoja wa abiria wawili alijeruhiwa vibaya baada ya kupigwa risasi, huku dereva wa gari hilo akifanikiwa kutoroka bila majeraha.

Visa hivyo viwili vimejiri wiki chache baada ya mashumbiliz sawia na hayo kutekelezwa na kusababisha vifo vya watu kadhaa na lori moja kuteketezwa, na washambuliaji wanaodaiwa kutoka nchi moja jirani.

TAGGED:
Share This Article