Abiria 21 wamefariki papo hapo na wengine watano kujeruhiwa baada ya gari la abiria kugongana ana kwa ana na lori kwenye barabara kuu ya Iringa – Mbeya nchini Tanzania mapema leo Jumatatu.
Taarifa kutoka kwa maafisa wa polisi wa Iringa imebainisha kuwa walioangamia ni pamoja wanaume 10, wanawake 9 na watoto wawili.
Taarifa za awali zinaashiria kuwa basi hilo la kampuni ya Maokoto, lilikuwa likisafiri kutoka kijiji cha Wasa mkoani Iringa kuelekea Mbeya.
Yamkini kufeli kwa breki za basi ndicho chanzo cha dereva wa basi hilo kupoteza mwelekeo na kugongana na lori.